Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Naibu Kamishana wa Polisi Zanzibar, Salum Msangi amesema tukio hilo lilitokea majira ya saa 7:40 usiku.


Amesema watu wengi ambao idadi yao haijajulikana baada ya kukivamia kituo hicho, walimfunga kamba mtangazaji wa zamu aliyejulikana kwa jina la Ally Abdallah na kumtoa nje kisha kukichoma moto kituo hicho.


Jeshi la polisi bado linaendelea na uchunguzi mkali kufauati tukio hilo.



No comments:
Post a Comment