.

.
TZ WAKA BLOG TUNAKUTAKIA HERI YA MWAKA MPYA 2016, MWAKA HUU UWE WA BARAKA NA MAFANIKIO KWAKO | KUTANGAZA NA BLOG HII WASILIANA NASI KUPITIA 0716 979 939 AU BARUA PEPE tzwakablog@gmail.com

GWAJIMA: NITAFANYA MKUTANO KWA SAA MOJA TU.

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, ameibuka na kusema atafafanua kila kitu kwa umma kuhusu madai yaliyotolewa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, dhidi yake wakati atakapozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaa kesho.

Amesema moja ya ufafanuzi atakaotoa ni kuhusiana na kubatizwa jina la mshenga na Dk. Slaa wiki iliyopita.  

Dk. Slaa alitoa kauli ya kumuita Askofu Gwajima kuwa mshenga Jumanne iliyopita wakati akizungumza na waandishi wa habari, akidai ndiye aliyekuwa amepewa kazi ya kuwaunganisha kati yake na mgombea urais aliyesimamishwa na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kupitia Chadema, Edward Lowassa.

Gwajima alisema atazungumza na waandishi wa habari kesho kwenye hoteli ya Landmark wakati wa ibada iliyofanyika kwenye kanisa la zamani la Ufufuo na Uzima lililopo Ubungo Maji, jijini Dar es Salaam, ikiwa ni wiki yake ya pili tangu alipohamia kwenye kanisa hilo baada ya kuhama kutoka viwanja vya Tanganyika Packers alikokuwa akitoa huduma hiyo. 

Alisema kwenye mkutano wake na vyombo vya habari atafafanua kuitwa mshenga, jambo ambalo asingeweza kuzungumza kwenye nyumba ya ibada.

“Najua hapa kuna waandishi wa habari wamekuja kujua nilivyokuwa mshenga, lakini kanisa langu siyo sehemu ya majibizano, bali nitafanya mkutano kwa saa moja tu inatosha kabisa kufafanua," alisema.

“Wakati nakuja kanisani nilipofika hapa maeneo ya Ubungo kwenye stendi za daladala, watu waliibuka na kuanza kupiga kelele wakiniita mshenga, mshenga, sasa hii ni ishara tosha, maana ndoa bila mshenga haiwezi kuwa ndoa na mshenga ndiyo mwenye jukumu la kuunganisha kuwa kitu kimoja na ikitokea kuna ugomvi ndiye anayesuluhisha,” alisema na kuongeza:

“Lakini niwaeleze kitu, si mnakumbuka yule Dokta Willibrod Slaa, aliyekuja kupiga magoti hapa mbele ya madhabahu ya kanisa hili Januari Mosi, mwaka huu?" Alisema na waumini wakashangalia huku wakipiga kelele na kusema "sema babaaaaa.”

Alisema mwanzoni mwa Januari, mwaka huu, kanisa hilo lilifunga siku 30 kwa ajili ya kutafuta kiongozi wa kuongoza nchi na kuwaeleza waumini wake kuwa kiongozi atakayeapishwa mwaka huu kuwa Rais, atakuwa pamoja nao kwa kuwa walifunga na kuomba, hivyo atakuwa amechaguliwa na Mungu. 

“Hivi mlishawahi kuona mtu anasimama kwenye vyombo vya habari na kusema mambo haya, ukiona dalili kama hizi ujue kwamba ndiyo tayari wameshakwisha," alisema.

No comments: