Leo Chama cha Kizalendo ACT Leo Kilizindua kampeni za urais, ubunge na udiwani katika viwanja vya Zakheem Mbagala kuanzia saa nane mchana hadi saa kumi na mbili jioni. Pia kilikuwa live katika TBC, AZAM, na ITV kuanzia saa tisa alasiri...hizi ni baadhi ya kauli zilizotolewa na Viongozi na wagombea wa Chama hicho.
Mshauri wa Chama - Prof. Kitila Mkumbo
"Jana nimesikia mtu mmoja anasema kuwa eti urais ni kama meneja.Kwa taaluma niliyonayo naomba niwaambie kazi za rais.
Hapa hatutafuti watu wa kusimamia miradi, hatutafuti watu wa kuzibua mitaro ila tunatafuta rais wa kutoa dira" alisema Prof. Kitila Mkumbo na kuanza kuchanganua kwa kina.
Kazi za Rais
1. FIKRA - Rais ndiye anayepaswa kutoa dira ya nchi,ili aweze kutoa dira lazma awe na fikra.Hawa mnaowasikiliza muwapime hapa.Huyo anayekuja na kusema nikiwa rais nitaleta maji huyo ni muongo labda kama atakuwa afsa mradi maji
Rais atakayekuja na ukamuuliza atakufanyia nini akasema ngoja nikasome ilani huyo wa kumuogopa ni muongo.
2. Rais ndiye mlinzi mkuu wa Tunu za TAIFA
Kuna tunu mbalimbali lakini za msingi ambazo ni...
- Mlinzi wa Umoja wa Taifa
- Mlinzi wa usawa katika taifa
- Muungano
- Uadilifu
- Demokrasia
3. Lazima awe mfano bora wa binadamu tunayemtaka katika jamii.
Rais tunayemtaka lazma aweze kuwawakilisha watanzania hata huko
4. Muadilifu, rais wetu lazma atokee chama cha kisiasa na ili awe muadilifu lazma chama anachotoka lazma kiwe na uadilifu.Rais anayetoka chama cha kilaghai,chama kinachotaka mafanikio ya haraka huyo hafai.Kama anatoka chama cha kilaghai basi naye atakuwa Laghai.
"Uchaguzi huu utakuwa uchaguzi wa Mbwembwe,ulaghai au unachagua misingi na sera, vyama vingine vinauza mbwembwe na ulaghai,sisi tunauza Misingi na Sera." Alimaliza prof. Mkumbo.
Kiongozi wa Chama - Mwami Zitto Kabwe
"Nampongeza kampeni meneja kwa maneno yake yanayotofautisha kati ya washindani na wenye nia
Naona kuna sehemu moja amezidiwa na kuongelea ugonjwa, naomba nichukue nafasi hii kwa niamba kuomba msamaha.
Mimi leo sio siku yangu ila ni siku ya mama Anna. Kampezi zetu ni UTU,UZALENDO na UADILIFU (Anaelezea kipengele kimoja kimoja)
Kila chama kinachogombea kimesema kitapambana na rushwa na ufisadi lakini hawajasema watapambana vipi, ACT Wazalendo pekee ndio kimesema kitapambana kwa kurejesha MIIKO na UADILIFU.
Nchii hii imeongozwa na mawazili wakuu wengi na mpaka sasa watatu wametangulia mbale ya haki ambao ni mwalimu Nyerere, Sokoine na Kawawa.... Mawaziri wakuu wanne wako CCM, Sumaye na Lowassa wako Ukawa na Malecela hajataja upande wake.
Hatuwezi kuleta mabadiliko kwa kurudisha watu wale wale ambao walituletea kadhia kwenye nchi.
Chama chenye uwezo wa kuleta mabadiliko (Changes with Content) ni ACT wazalendo pekee ndio maana tumewaletea mama. Nchii hii imeongozwa na marais wanne na kumekuwepo na ufisadi wa kutisha, ACT wazalendo tumewaletea mama ili aweze kukabiliana na ufisadi huu.
Wagombea waliopita wamesema watatoa baadhi ya huduma bure kama elimu, lakini hawatuambii pesa watatoa wapi hizo pesa za kuendesha elimu bure.
CCM wamesema watatoa 50ml kwa kila kijiji ambazo ni pesa nyingi,lakini hawajasema watatoa wapi hizo pesa kama sio kuwabebesha wananchi mzigo wa kodi.
Nchi yetu inapoteza kodi zaidi ya bilioni 600 kila mwaka kwasababu baadhi ya wafanyabiashara wanakwepa kodi.Sio CCM wala UKAWA wanaweza kuwataja maana ndio wafadhili wao wakubwa wa kampeni.
ACT wazalendo mkimpitisha mama msiulize tutapata wapi hela za kutoa huduma hizo, mama ataziba mianya yote ya Rushwa na pesa zitapatikana na kuwekezwa kwenye miradi.
Tunaambiwa ufisadi sio ajenda,wakati huu wa kampeni kuna watu wanaendelea kupiga pesa, juzi hapa kuna kampuni kutoka Switzeland kuna kampuni imepewa tenda na tenda ile haikutangazwa, katika tenda hiyo wapigaji watapata zaidi ya bilioni 20. Chagueni ACT wazalendo ili ajenda ya Ufisadi tuweze kuisimamia
Kwenye ilani yeti tumesisitiza uzalendo,tumesisitiza tutawafanyia nini watanzania.Mgombea na mgombea mwenza watakuja kueleza ndani ya muda mchache ujao.
Tarehe 5 mwezi ujao, timu yetu ya taifa itacheza na timu ya Nijeria,nawaomba TFF wawaruhusu wananchi wakaishangilie timu yao bure. Mipango yetu ni kuhakikisha kuwa timu ya Taifa inacheza kombe la dunia.
Magufuli mlishawahi kumuona Taifa, mtu kama huyo kweli anaweza kukuza michezo? ACT wazalendo ndio pekee tunaweza kukuza michezo na ndio maana nawaambia Jumamosi wote tukutane Uwanja wa Taifa Tukaishabikie timu ya Taifa ili ishinde na kuingia hatua ya pili."
Seleman Msindi (Afande Sele)
Siku mkiona naapishwa kuwa mbunge basi kila mmoja aseme kuwa Chizi kalogwa tena, sasa nawakaribisha mgombea urais na Mgombea mwenza
Mgombea mwenza - Hamid Yussuf
"Nnayo hekima kubwa kusimama mbele yenu,namshukuru Mngu kunipa hekima hii, nawashukuru viongozi wa Chama na wanachama kwa kuniamini na kunipa nafasi hii.Tatu nachukua nafasi hii kuwapa shukrani wazazi wangu ambao wametangulia mbele ya haki.mwisho mke wangu ambaye amenivumilia kipindi chote nawatumikia watanzania.
Miez miwili ijayo naenda kuapishwa kuwa makamu wa rais wa Tanzania na nakwenda kufanya kazi,siendi kuwa mzibua mitaro.
Kuna wagombea wanaogopa mabadiliko lakini napenda kuwahakikishia kuwa yaliyotokea Tunisia ni pale kijana aliyemaliza masomo yake baada ya kukosa ajira akajiajiri lakini alikamatwa na manispaa ndio akajimwagia mafuta na kujichoma na ndipo mabadiliko yalioanzia na mpaka sasa mambo shwari.
Sitaki yatokee mabadiliko kama Tunisia ila sisi mabadiliko yetu yawe kwenye boksi la kura ili act wazalendo tuweze kuingia ikulu na kuwatumikia watanzania."
Mgombea Urais - Anna Mghwira
Anawashukuru watanzania
"Nasimama mbele yenu kuomba ridhaa kwenu watanzania ili niweze kuwa rais wenu.Watanzania ni sehemu ya vijana na wazee,wanawake na waume
Mkinipa ridhaa nitaunda serikali umoja itakayotokana na viongozi wazalendo,waadilifu watu kutoka sekta binafsi ila wawe waadilifu,wazalendo ili kuunda taswira ya nchi yetu.
Kwenye kujenga Taifa hakuna hitakadi ya udini wala jinsia bali utaifa.
Serikali yetu ikiundwa italeta vipaumbele vyake mapema, serikali yetu itahamishiwa Dodoma na sio makao makuu ya Chama.Tutaamua makao makuu ya Chama yawe mkoa gani.
Dodoma maana yake ni kuwaletea umoja wananchi wetu.Chama chetu kimeweka na mimi natasimamia ili kufanikisha.
Chama chetu kimekuja na vipaumbele vikuu vinne...
1. Hifadhi ya Jamii
2. Uchumi shirikishi na wenye kuzalisha ajira nyingi na bora. Baada ya kuingia madarakani tutaruhusu tume ya Warioba imalizie mchakato
3. Afya, Tanzania ina mfumo mbaya wa huduma za afya, chini ya ACT itahakikisha kila mtanzania anafahamika alipo na huduma zinamfika.
4. Elimu, watoto wanamaliza shule hawajui kusoma na kuandika, mwanafunzi wa chuo kikuu anashindwa kujieleza, ACT tutajitahidi kunua vipaji, leo tumezalisha watoto wa mitaani."
No comments:
Post a Comment