
Kaimu Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Sokoine ya Mkoa wa Lindi, Damasiana Msalla akimuongoza Naibu Waziri wa Afya, Maendejana ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla kuelekea kwenye wodi za hospitali wakati wa ziara ya kushtukiza aliyofanya mkoa wa Lindi.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Sokoine ya Mkoa wa Lindi, Dkt. Evaristo Kasanga akimkaribisha Dkt. Hamisi Kigwangalla alipotembelea wodi za hospitali hiyo wakati wa ziara ya kushtukiza aliyofanya jana mkoa wa Lindi.Katikati ni Mganga wa Meno na Kinywa katika hospitali hiyo, Dkt. Hussein Athumani.

Mtaalamu wa Tehama katika Hospitali ya Sokoine ya Mkoa wa Lindi, Abdallah Kivurugo akitoa maelekezo kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendejana ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla (kulia) namna wanavyomsajili mgonjwa anapofika hospitalini hapo wakati wa ziara ya kushtukiza aliyofanya jana mkoa wa Lindi.

Naibu Waziri wa Afya, Maendejana ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla (kulia) akihoji jambo kwenye chumba cha mapokezi katika Hospitali ya Sokoine ya Mkoa wa Lindi, wakati wa ziara ya kushtukiza aliyofanya jana mkoani humo
No comments:
Post a Comment