Mshambuliaji Nyota wa Kimataifa wa Nigeria Gbolahan Salami, ametolewa kwenye Kikosi cha Eagles Squad kinachotarajiwa Kucheza na Taifa Stars-Tanzania kwa ajili ya mechi muhimu ya kufuzu kuingia kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Jumamosi hii jijini Dar es Salaam.
Chanzo hicho cha Habari Kutoka ndani ya kikosi hicho kilisema kuwa Sababu kubwa Kucheleweshwa kutolewa kwa Hati ya Kimataifa ya Kusafiria ya Mshambuliaje huyo na Ubalozi wa Norway jijini Lagos ndio kitu kikubwa kinachomsumbua mchezaji huyo kwa sasa.
"Akili ya Salami haikuwa mazoezini alipokuwa kambini, anahitaji sana kuhamia Nchini Norway, hivyo Ucheleweshwaji wa Kutolewa kwa Hati yake ya kusafiria na Ubalozi wa nchi hiyo kumemsababisha kukosa raha kabisa na kupelekea akili yake kushindwa kuzingatia mazoezi tukiwa kambini na hiyo ndio sababu kubwa iliyomfanya Kutolewa rasmi kwenye kikosi hicho " Kilisema Chanzo hicho cha Habari na kuendelea kueleza kuwa
"Gbolahan Salami amekuwa akipigania sana nafasi hiyo ya kwenda nje kujisajili kucheza Nchini Norway kabla ya Dirisha la usajili halijafungwa hivyo ni vyema kwa Mchezaji huyo kuwa makini wakati mwingine atakapoalikwa na The EAGLES."
Wakati huohuo Mshambuliaji mwngine wa Super Eagle Obafemi Martins. anaamini kuwa timu itakuwa katika ubora wake itakapokuja kucheza Dar es Salaam kutokana na wachezaji walioalikwa na Kocha Sunday Oliseh.
"Nafikiri Kocha amechagua kikosi kizuri sana na Natarajia NIGERIA tutashinda dhidi ya TANZANIA" alisema kutoka katika ngome yake ya Seattle USA
"Hatutakiwi Kudharau Kiwango cha timu yoyote ya Afrika kwa sasa; Hakuna kosa dogo kwenye mpira, Nimeona orodha ya wachezaji tutakaokuwa nao wana uzoefu wa kutosha wakiongozwa na EMENIKE (Emmanuel) pamoja na Vincent Enyeama na nina uhakika timu yetu itawapiga wenyeji Tanzania na kuibuka kiongozi wa Kundi" Alimaliza Obafemi
No comments:
Post a Comment