.

.
TZ WAKA BLOG TUNAKUTAKIA HERI YA MWAKA MPYA 2016, MWAKA HUU UWE WA BARAKA NA MAFANIKIO KWAKO | KUTANGAZA NA BLOG HII WASILIANA NASI KUPITIA 0716 979 939 AU BARUA PEPE tzwakablog@gmail.com

Mchezo mgumu wa Simba

https://ramadhaniabubakari.files.wordpress.com/2013/10/dsc_0020.jpg?w=1075
SIMBA leo inacheza na Coastal Union ya Tanga kwenye Uwanja wa Mkwakwani katika mfululizo wa Ligi Kuu Tanzania Bara. 

Ni mchezo unaotarajiwa kuwa mgumu kwani unakutanisha timu ambazo moja inaongoza ligi ikiwa na pointi 54 ikipania kutwaa ubingwa na nyingine inashika nafasi ya mwisho kati ya timu 16 zinazoshiriki ligi hiyo ikiwa na pointi 19.

Licha ya kushika mkia, lakini Coastal Union ilionesha uwezo mkubwa katika michezo yake iliyocheza katika uwanja wake wa nyumbani hivi karibuni dhidi ya timu nyingine zilizopo kileleni mwa msimamo wa ligi, ambapo iliifunga Yanga mabao 2-0 na kisha ikaifunga Azam bao 1-0.

Yanga inashika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 50 sawa na Azam inayoshika nafasi ya tatu, isipokuwa zinatofautiana uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa. Ni wazi Coastal Union haitakubali kuadhirika nyumbani, kwani kupoteza mchezo leo kutaiweka katika nafasi mbaya zaidi kuepuka janga la kushuka daraja.

Kama Simba itashinda leo itafikisha pointi 57 na kuweka pengo kubwa la pointi dhidi ya Yanga na Azam ingawa yenyewe itakuwa mbele kwa michezo mitatu. 
Mechi nyingine za ligi hiyo leo ni Kagera Sugar na Mtibwa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Tabora, Majimaji itakuwa mwenyeji wa Mbeya City Uwanja wa Majimaji Songea na Stand United itaikaribisha Ndanda FC Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

No comments: