
Peter amewataja Ruge Mutahaba, Master Jay, Ditto, Barnaba na wengineo ndio waliokuwa wa mwanzo kumwambia ukweli wa mapungufu yaliyokuwa yakikwamisha kufanya vizuri kwenye nyimbo alizotoa.
“Mtu wa kwanza kabisa ni Ruge, aliniita kabisa personally akaniambia we msechu unauwezo mkubwa sana wa kuimba lakini njia unayoenda sio. Mtu mwingine ni Ditto aliniita kwamba Msechu unakosea. Master Jay hata kwa mfano ukiangalia ile ‘Hasira Hasara’ Master Jay alinielekeza vizuri sana. Kuna mtu mwingine anaitwa Richard Horombe ambaye alishawahi kuwa hata meneja wangu, Kuna mtangazaji wa Magic Fm anaitwa Tee Jay alishanifata akaniambia Msechu unapiga kelele unashout, don’t shout. Mwasiti, Barnaba mwenyewe pia alishaniambia unaimba vitu vingi blaza calm down mbona kama unapanic hivi. Kidumu, Ray K, kuna Kavuta alikuwa n voice coach wa Tusker Project Fame alishanipigia hadi simu Peter mbona umeachia nyimbo yako mbona unashout masikioni, kwahiyo watu kama hao walinisaidia sana”, alisema Msechu kupitia Amplifaya ya Clouds Fm.
Msechu amesema toka achukue uamuzi wa kutoandika tena nyimbo zake ameshanunua na kauandikiwa nyimbo zaidi ya sitini hadi sasa.
No comments:
Post a Comment