.

.
TZ WAKA BLOG TUNAKUTAKIA HERI YA MWAKA MPYA 2016, MWAKA HUU UWE WA BARAKA NA MAFANIKIO KWAKO | KUTANGAZA NA BLOG HII WASILIANA NASI KUPITIA 0716 979 939 AU BARUA PEPE tzwakablog@gmail.com

21 September, 2015

RAIS KENYATTA: HATUWEZI KULIPA WALIMU

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.
Wakati shule zote za serikali na za binafsi nchini Kenya zikianza kufungwa kuanzia hii leo, rais wa nchi hiyo, Uhuru Kenyatta akihutubia taifa hilo kwa njia ya televisheni amesisitiza kuwa serikali yake haina uwezo wa kulipa nyongeza ya mishahara wanayodai waalimu wanaoendelea na mgomo.
Mgomo wa walimu nchini Kenya
Ametoa wito kuwa, mgogoro huo utatuliwe kwa amani na kusema kuwa shule zote zinafungwa kuanzia leo. Serikali ya Kenya imeagiza shule zote nchini humo zifungwe kuanzia leo huku mgomo wa walimu nchi nzima ukiendelea.
Barua kutoka kwa wizara ya elimu imeagiza shule zote za serikali na za kibinafsi zifungwe na wanafunzi warudi majumbani mwao. Watakaosalia shuleni pekee ni wanafunzi wanaojiandaa kufanya mitihani ya kitaifa ya darasa la nane na kidato cha nne mwaka huu.

No comments: