Wakati ujumbe huo umeanza kusambazwa nilikuwa kwenye mikutano ya Kampeni ya Mgombea Mwenza wa CCM Mhe. Samia Suluhu Hassan Wilayani Nachingwea na Liwale hivyo kupelekea kuchelewa kutoa taarifa yangu hii.
Napenda kuufahamisha umma kwamba ujumbe huo uliosambazwa ni wa uwongo na hapajawahi kuwepo mawasiliano hayo popote. Ni ujumbe uliotengenezwa kuupotosha umma kwa manufaa ya kisiasa ya walioutunga na kuusambaza.
Vilevile, napenda kuujulisha umma kwamba Mimi binafsi situmii njia ya mawasiliano ya whatsapp na wala sijawahi kuitumia wakati wowote ule, hivyo siwezi kuwa kwenye group lolote lile kama ujumbe uliosambazwa ulivyotaka kuuhadaa umma.
Ni vema ikaeleweka kuwa ni kosa la Jinai kujifanya wewe ni mtu fulani wakati siyo. Hivyo naviomba vyombo vya sheria kuwasaka wahusika na kuwachukulia hatua za kisheria waliotunga na kusambaza ujumbe ule kwa kutumia majina ya watu wengine.
Natumaini TCRA nao watafuatilia chanzo cha taarifa hizo za uwongo ili washughulike na wahusika kupitia sheria ya makosa ya mtandao.
Ninawapa pole wale wote waliopata usumbufu kutokana na taarifa hizo za uwongo.
No comments:
Post a Comment