.

.
TZ WAKA BLOG TUNAKUTAKIA HERI YA MWAKA MPYA 2016, MWAKA HUU UWE WA BARAKA NA MAFANIKIO KWAKO | KUTANGAZA NA BLOG HII WASILIANA NASI KUPITIA 0716 979 939 AU BARUA PEPE tzwakablog@gmail.com

22 December, 2015

COSOTA yataja kiasi atakacholipwa msanii kwa kila wimbo au video itakayotumiwa na radio au TV!

Maswali mengi yanayoendelea kuulizwa baada ya sheria mpya kutangazwa ya wasanii kulipwa na vyombo vya habari  kuanza kuwalipa wasanii wasanii kwa kucheza nyimbo zao kuanzia mwakani (2016), ni pamoja na kiasi gani msanii atakuwa analipwa.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA), Doreen Sinare alisema alisema kuwa wanamuziki, watunzi na maproducer watalipwa asilimia 60 kwa kila wimbo au video itakayochezwa katika redio na televisheni yoyote ndani na nje ya nchi kwa kutumia vifaa bora vilivyowekwa na kampuni ya CMEA.
Doreen alisema mwanamuziki, msanii alitakiwa kulipwa asilimia 70 ya kazi yake, lakini asilimia 10 itakatwa katika malipo hayo na kuingia katika mifuko ya jamii kwa mahitaji yake ya baadaye.
Alisema mwanamuziki ni sawa na wafanyakazi wengine na asilimia 10 ya hiyo itamwezesha kujipatia kipato chake kama ilivyo kwa wafanyakazi wengine katika taasisi mbalimbali.
COSOTA kwa kushirikiana na kampuni ya kazi za wanamuziki nchini Copyrights Managements East Africa Limited (CMEA) wataanza kulipa mirahaba ya wanamuziki na wadau wake kuanzia mwakani.

No comments: