.

.
TZ WAKA BLOG TUNAKUTAKIA HERI YA MWAKA MPYA 2016, MWAKA HUU UWE WA BARAKA NA MAFANIKIO KWAKO | KUTANGAZA NA BLOG HII WASILIANA NASI KUPITIA 0716 979 939 AU BARUA PEPE tzwakablog@gmail.com

15 March, 2016

RAIS KAGAME ASEMA YUKO TAYARI KUIGA NYAYO ZA MAGUFULI

 
Hatimaye Rais wa Rwanda, Paul Kagame, ameahidi kuiga mfano wa Rais John Magufuli, kwenye jitihada za kutokomeza ufisadi nchini mwake, ikiwa ni pamoja na kusitisha ziara za mawaziri alizozitaja kuwa zinafuja mali za taifa.

Rais Kagame aliyasema hayo mwishoni mwa wiki kwenye mkutano wa 13 wa faragha wa viongozi wa taasisi zote za serikali nchini humo, akiahidi kujifunza na kutumia sanaa ya kupunguza matumizi ya fedha za serikali kama anavyofanya Magufuli.


“Ninajifunza kutoka kwa 'tingatinga' la Tanzania, Rais John Pombe Magufuli, lakini nina ushujaa wa kukaza mambo zaidi,” alisema.


Kagame alisema suala la ufisadi nchini humo linachukua mwelekeo mpya na kasi ya ajabu, na kwamba hawezi kuendelea kulivumilia tena.
Akiwa ameambatana na mkewe mama Jeannette Kagame, kiongozi huyo alitahadharisha juu ya safari zisizo na tija na matumizi yasiyo ya lazima ya maofisa wa serikali.

No comments: