.

.
TZ WAKA BLOG TUNAKUTAKIA HERI YA MWAKA MPYA 2016, MWAKA HUU UWE WA BARAKA NA MAFANIKIO KWAKO | KUTANGAZA NA BLOG HII WASILIANA NASI KUPITIA 0716 979 939 AU BARUA PEPE tzwakablog@gmail.com

KANUSHO LA TAAARIFA



Takribani siku mbili zilizopita zilienea taarifa juu ya katazo rasmi la mavazi ya nguo fupi ambalo ilisemekana limetolewa na wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Kupitia tovuti ya Wizara Sambamba  na  mahojiano kupitia Power Breakfast asubuhi ya leo, waziri mwenye dhamana ya Wizara hiyo, Mh Nape Nnauyeamekanusha juu ya taarifa hiyo.

"Taarifa hizo si za ukweli, nasikitika sana watu wanatuma taarifa hiyo kwenye mitandao tofauti ya kijamii, Wizara imesikitika kwa kusambazwa kwa Taarifa hiyo ikianisha picha ya mavazi ambayo yamepigwa marufuku, naomba chombo kinachohusika kichukue hatua dhidi ya watu waliohusika na taarifa hiyo potofu ili watu wengine wajue sheria inafuata mkondo wake.Mh. Nape Nnauye.


Tangazo hilo lilisema:
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
Napenda kuwafahamisha wananchi wote ifikapo January 2016 mavazi yote yasiyostahili ambayo hayaendani na mila, desturi zetu Wizara yangu na serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania haitafumbia macho mavazi hayo.

HAYARUHUSIWI KUVALIWA SEHEMU ZIFUATAZO;

  1. Kwenye masoko makubwa
  2. Hospital kubwa (Private or Publick)
  3. Maofisini na Vyuoni
  4. Mijini kwenye mkusanyiko wa watu wengi

Hatua kali za kisheria zitachukulikwa endapo kwa wale ambao watavaa haya; ikiambatana na fine ya Tshs 100,000/+

No comments: