.

.
TZ WAKA BLOG TUNAKUTAKIA HERI YA MWAKA MPYA 2016, MWAKA HUU UWE WA BARAKA NA MAFANIKIO KWAKO | KUTANGAZA NA BLOG HII WASILIANA NASI KUPITIA 0716 979 939 AU BARUA PEPE tzwakablog@gmail.com

11 November, 2015

Askari mtuhumiwa wa rushwa afutwa kazi



JESHI la Polisi mkoani Tanga limemfukuza kazi askari wa kikosi cha usalama barabarani aliyetambulika kwa namba F. 785 CPL Anthony Temu (46) wa kituo cha Polisi Kabuku kwa kosa la kufedhehesha jeshi hilo.


Akitoa taarifa kwa vyombo ya habari ofisini kwake Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga, Zuberi Mwombeji amesema askari huyo amefukuzwa baada ya kuthibitishwa kwa taarifa iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonyesha akiomba na kupokea rushwa wakati akitekeleza majukumu yake.

Video hiyo  ilichukuliwa eneo la Kabuku, Tanga na kusambazwa WhatsApp na kesho yake ndipo Askari Huyo alitangazwa kuwa amefutwa kazi

No comments: