.

.
TZ WAKA BLOG TUNAKUTAKIA HERI YA MWAKA MPYA 2016, MWAKA HUU UWE WA BARAKA NA MAFANIKIO KWAKO | KUTANGAZA NA BLOG HII WASILIANA NASI KUPITIA 0716 979 939 AU BARUA PEPE tzwakablog@gmail.com

22 November, 2015

MATUMAINI YA WATANZANIA KWA VIONGOZI HAWA WAKUU WA SERIKALI TANZANIA YASIHUJUMIWE NA SIASA.



Tangu kumalizika kwa Zoezi la uchaguzi Mkuu Tanzania Bara, na Rais Dr. John Pombe Magufuli, kuchaguliwa na kuapishwa  kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa na Makamu wa Rais wa Kwanza Mwanamke Mh. Samia Hassan Suluhu, na hatimaye Juzi Rais Kumteua tena Mh. Majaliwa kuwa Waziri mkuu wa Tanzania kwa Serikali yake ya Awamu ya Tano....Wananchi wameendelea kujenga Matumaini tele kwa namna Serikali ya Awamu ya Tano kutokana na jinsi ilivyoanza kufanya kazi kwa kuonyesha kufahamu Mianya yote inayohujumu na kushusha maendeleo nchini na kuahidi kupambana nayo.

Rais Magufuli aliibua  Mjadala zaidi kwa watanzania wengi Pale alipolihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mara ya kwanza Novemba 20,2015.

Mbali na Kuomba Ushirikiano kwa bunge hilo, lakini pia alielezea Namna ambavyo uongozi wake umejipanga Kushughulikia masuala mbalimbali na kugusia vitu kama uwajibikaji wa watendaji wa serikali, Upigaji vita Rushwa, ubinafsi na ufisadi, na Kuwatumikia wananchi kwa nguvu ili taifa liweze kusomba mblele, sambamba na kutoa agizo la fedha zilizochangwa na wafadhili kwa ajili ya Cocktail ya ufunguzi wa Bunge kutoka Tsh. 276Millioni hadi Tsh. 25Millioni, akitoa maelezo ya kuwa .."Wabunge hawawezi kufanya Cocktail Party ya Tsh. 276Million wakati kuna watu wanalala chini hospitali". 

MASWALI YA KUJIULIZA?

Mara Baada ya Kauli hiyo kutolewa Bungeni Mapema Juzi, Zilianza Kusambaa Picha za Vitanda vya Wagonjwa kwenye mitandao kuwa taayari vimeanza kuwasili katika Hospitali ya taifa muhimbili..
 
Ukweli ni kwamba Baadhi ya Wananchi wamejilazimisha kuamini kuwa hizi picha zinazosambaa ni za hivi karibuni, na kama ni kwa tukio la leo, kufuatia agizo lililotolewa juzi, what was the scenario katika suala zima la govt procurement procedures? Does it mean kuwa umefanyika mpango wa dharura, kwa single sourcing, ama kwa namna gani?

Secondly, yaani vitanda vya wagonjwa, magodoro na wheelchairs nowdays ni one of fast moving consumables hapa kwetu kiasi kwamba I can just wake up one morning na kumtuma kijana kwenda kununua 100+ pcs na akarudi navyo jioni? Nina hakika hata kwa anayetala vitanda vya mbao pale keko, if by any reasons na any pressure akahitaji 50 tu, of the same specifications, lazima itambidi aweke "order" na the same kuwa delivered in about a week time or more.

Sasa hivi tunavyoaminishwa, I swear I wanna be the first to believe, vimekuwa sourced wapi, kwa agreement ama LPO iliyotayarishwa muda gani etc?

Mbali na hivyo, in some pics, tumeona Lorry la MSD, ama vilikuwa stoo kwao vikisubiri agizo? Yaani viliwekwa stoo since lini na kwa matumizi yapi?

Binafsi bado nina mashaka tele kuhusiana na hili. Si kwamba sikubaliani na agizo, naamini linatekelezeka, ila napata shida kusadiki uhusishwaji wa hizi picha na agizo ya jana. Hata kama ndio Fast-Forward (F/F) ile ya kwenye audio tapes za zamani, hii ni supersonic speed.

All in all, this is too good to be true....Viongozi wetu wanajitahidi kujenga Tanzania Mpya na kupunguza propaganda za utendaji, Tafadhali Tusihujumu Imani ya Watanzania kwa Viongozi wetu Wakuu wa Serikali kwa Propaganda za kisiasa, kama ni kweli hili Limeshatekelezwa Muhimbili itolee ufafanuzi wa Utaratibu uliotumika ili wananchi waelewe.

No comments: