
Katika uteuzi huo, mawaziri wateule 13 walikuwamo katika Baraza la Mawaziri la Serikali ya awamu ya nne chini ya Rais mstaafu, Jakaya Kikwete, huku wapya wakiwa wawili ambao ni Balozi Dk. Augustine Mahiga na Nape Nnauye.
Kwa upande wa manaibu waziri, wengi ni sura mpya ambazo hazikuwamo katika Baraza la Mawaziri la Serikali ya awamu ya nne.
Uamuzi huo wa Rais Magufuli, kutangaza baraza lake la mawaziri, sasa unavunja ukimya na maswali ya muda mrefu kuhusu uundwaji wa baraza hilo.
Rais Magufuli, amesema pamoja na hali hiyo hata akikamilisha uteuzi wa wizara nne zilizobaki, baraza lake la mawaziri litakuwa na mawaziri 34 tu tofauti na Serikali ya awamu ya nne chini ya Rais mstaafu Jakaya Kikwete, iliyokuwa na mawaziri na manaibu waziri 60
No comments:
Post a Comment