18 December, 2015
UMEWAHI KUSIKIA KUHUSU MWALIMU MSTAAFU "SANDWICH MAN" ANAYEJITOLEA KUZUNGUKA MITAANI KUGAWA MIKATE 520,000 KWA WASIO NA MAKAZI MINNEPOLIS MAREKANI
Allen Law hutumia karibu kila siku Usiku kuzunguka mitaa mbalimbali ya jiji la Minnepolis mara baada ya kazi zake za kufundisha shule kama Mwalimu, hata baada ya Kustaafu bado aliendelea na moyo wa kufanya hivyo...
Taarifa zake zilisambaa sana mwaka 2014 katika mitandao mbalimbali ikionyesha jinsi nyumba yake ilivyokuwa na majokofu (Fridges) mengi ya kuhifadhia vyakula na sakafu ya nyumba yake ikiwa imejaa Rundo la Mikate..
Mbali na daktari wake kumuonya juu ya afya Umri na hatari inayoweza kuikumba afya yake akikosa usingizi wa kutosha bado Allen Hupata muda mchache zaidi wa kulala na kufanya yote haya peke yake akiwa na gari lake bila ya msaada kutoka kwa mtu yeyote na bila ya kutarajia malipo.
"Mbali ya Kiasi kdogo cha uwezo unachoweza kuwa nacho, bado unaweza kuwa na Msaada wa Kuwafaa wengine."- Kauli ya Allen law
Labels:
Zaidi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment