.

.
TZ WAKA BLOG TUNAKUTAKIA HERI YA MWAKA MPYA 2016, MWAKA HUU UWE WA BARAKA NA MAFANIKIO KWAKO | KUTANGAZA NA BLOG HII WASILIANA NASI KUPITIA 0716 979 939 AU BARUA PEPE tzwakablog@gmail.com

13 September, 2015

Mbasha 'Amjibu Gwajima'


Siku chache baada ya Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima kujibu mapigo ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbrod Slaa, sasa Emmanuel Mbasha ambaye ni mume aliyetengana na mkewe, Flora Mbasha amerejea madai yake kwamba, Gwajima alisimamia mchakato mzima wa yeye na mkewe kutengana.

Akizungumza katika mahojiano ya takribani dakika thelathini, Mbasha alisema alimshuhudia Gwajima, Jumanne wiki hii akitupa shutuma kwa Dk. Slaa tena kwa kuyaanika mambo yake ya ndoa, yeye akashangaa sana.

"Na mimi leo nataka kumjibu Gwajima kama yeye naye alivyojitokeza kumjibu Dk. Slaa. Gwajima niliwahi kumshutumu kwa kuhusika na kuvunjika kwa ndoa yangu. Leo hii anasimama kwa kujigamba akisema Slaa si msafi, yeye ana usafi gani?.

"Lakini kiko wapi sasa! Hata huyo Flora mwenyewe ameshamkimbia, yuko kwingine. Kwa hiyo kama ishu ni uchafu, Gwajima pia si msafi. Ana mambo anajua alikuwa akiyafanya kwa mke wangu, mimi nayajua na nina ushahidi."

Hata hivyo, Mbasha hakufafanua, Flora amemkimbia Gwajima kivipi? Na huko kwingine alikokwenda ni kwa nani na kwa sababu gani!

ANA MAZITO YA GWAJIMA

Lakini alikwenda mbele zaidi kwa kusema: "Naomba leo niseme kwamba nina mambo mazito sana ya Gwajima ambayo siku ikifika nikienda kuyasema kanisani kwake waumini wake watashangaa wote. Muda bado haujafika lakini ukifika nitamlipua."

"Je, kuibuka kwako upya tukisema umetumwa na chama kimoja cha siasa umchafue Gwajima, utasemaje?"

Mbasha: "Kwani ye' alitumwa na nani? Mimi nimeibuka kwa sababu hata yeye ameibuka. Kama angesimama pale (ukumbi wa Hoteli ya Landmark) akasema mambo yake bila kukosoa ndoa ya Dk. Slaa hata mimi nisingepanua kinywa kusema. Hawezi kusema siri za mwenzake kama mtumishi. Tena anasema mpaka ishu ya Dk. Slaa kulala ndani ya gari."

"Nimeamua kusema kwa sababu yeye amemwona mwenzake si msafi. Yeye usafi wake ni upi? Niliachana na Flora, akaenda kwake, yeye akampokea. Angekuwa msafi angemshauri Flora kwamba alichofanya si kizuri. Hapo ningesema ni msafi."

Wakati Mbasha akirusha madai hayo huku akisema mkewe amemkimbia Gwajima na yuko kwingine, kwa upande wake, Flora aliwahi kusema: "Nina mambo kibao ya Mbasha, nikiyasema watu watashangaa! Lakini siku zote mimi namwachia Mungu tu. Yeye ndiye muweza wa yote.

GPL

No comments: