Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete jana alizindua Chuo cha Ukamanda kilichopo eneo la Duluti nje kidogo ya jiji la Arusha.
Uzinduzi huo ulifanyika ukiwa pia na Mkuu wa Chuo Cha Ukamanda na Unadhimu Meja Jenerali Ezekiel Kyunga, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, pamoja na mwakilishi kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu Balozi Ibrahim Al Suweidy.
umoja wa Falme za Kiarabu ulishirikiana na Serikali kufadhili ujenzi wa Chuo hicho.
No comments:
Post a Comment