.

.
TZ WAKA BLOG TUNAKUTAKIA HERI YA MWAKA MPYA 2016, MWAKA HUU UWE WA BARAKA NA MAFANIKIO KWAKO | KUTANGAZA NA BLOG HII WASILIANA NASI KUPITIA 0716 979 939 AU BARUA PEPE tzwakablog@gmail.com

07 November, 2015

MWANAMKE WA KITANZANIA APIGWA NA GLASI YA POMBE KWA KUZUNGUMZA KISWAHILI MAREKANI




Mwanamke mmoja raia wa marekani ameshtakiwa Mjini Minnesota kwa kosa la Kumsahambulia na kumjeruhi Mwanamke wa kiislamu Mtanzania (Asma jama) aliyekuwa akizungumza kiswahili kwenye Mgahawa wa chakula wa Applebee’s
Jodie Marie Burchard-RischJodie Marie Burchard-Risch ambaye usiku wa Oktob 30 alikuwa akipata chakula cha usiku na Mumewe Mgahawani hapo alionekana kukerwa na Mwanamke huyo Mtanzania  kuzungumza Kiswahili nyuma ya Meza aliyokuwa amekaa Imeripoti KARE-TV.
Burchard-Risch mwenye umri wa miaka 43 alisimama ghafla na kumfokea Mtanzania huyo kisha Kumtupia glasi iliyokuwa na Pombe ambayo ilipelekea Mtanzania huyo 'ASMA JAMA' Kuumia na kupata majeraha ya kuchanika maeneo kadhaa usoni.
Kuhusiana na tukio hilo Asma amesema kwamba “Nilikuwa Nimekaa na binamu zangu wadogo tukizungumza lakini ghafla wakati nageuka bila kujua kinachoendelea nilijikuwa Nikirushiwa kitu iliyonipiga kwa nguvu usoni, ndipo Binamu zangu ambao ni wadogo chini ya miaka 11 walipoanza kupiga kelele na kutaka kukimbia" 
Mwanamke huyo pia amesema kuwa anashangaa tukio hilo kwa sababu anayo haki ya kuongea na kuzungumza na familia yake Kiswahili.
Nao Polisi wamesema kuwa baada ya mwanamke huyo mmarekani Burchard-Risch kugundua kuwa ametenda kosa hilo alikimbia kabla ya kuzuia nje ya mgahawa huo hadi polisi walipofika na kumkamata.
Asma Jama baada ya tukio hilo alipata Majeraha makubwa ya kukatwa kuzunguka pua yake, Mboni ya jicho pamoja na sehemu ya chini ya mdomo.
“Binafsi tukio hili limeniumiza zaidi,” amesema Jama. “Nimeishi Minnesota kwa miaka 15, hakuna mtu aliyewahi kunishangaa kwa kutoongea Kiingereza au kuvaa Hijab, Nilikuwa nikishuhudia matukio kwenye televisheni lakini sasa limenitokea, Nimekuwa mtu wa tofauti sana, na sipendezwi na hali hii”
Burchard-Risch alishtakiwa na kupatikana na hatia ya kufanya shambulizi la kujeruhi.

No comments: