Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC - Legal and Human Rights Centre), Dk. Helen Kijo-Bisimba anaendelea vizuri baada ya kunusurika ajalini siku ya Jumapili, Novemba 8, 2015 majira ya asubuhi katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi jijini Dar es Salaam.
Gari hilo lilikuwa likiendeshwa na dereva wake ambaye. Majeruhi waliwahishwa katika hospitali ya Agha Khan jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa LHRC, Imelda Urio ameiambia ITV/Radio One Stereo kuwa Bi Bisimba na wenzake watatu waliokuwemo katika ajali hiyo wanaendelea vizuri na wengine wanaweza kuruhusiwa kurudi nyumbani.

No comments:
Post a Comment