.

.
TZ WAKA BLOG TUNAKUTAKIA HERI YA MWAKA MPYA 2016, MWAKA HUU UWE WA BARAKA NA MAFANIKIO KWAKO | KUTANGAZA NA BLOG HII WASILIANA NASI KUPITIA 0716 979 939 AU BARUA PEPE tzwakablog@gmail.com

12 September, 2015

 TAARIFA KWA WATOA HUDUMA ZA UTANGAZAJI


Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inapenda kutoa taarifa kuwa kuanzia leo tarehe 10 Septemba 2015, na katika kipindi chote cha kampeni za uchaguzi  mkuu 2015, watu ambao sio wagombea wa udiwani, ubunge, urais, wasemaji rasmi wa vyama au watu wasioteuliwa na vyama vya siasa kama wawakilishi hawataruhusiwa kushiriki katika vipindi vya moja kwa moja (Live Programmes) vinavyohusu shughuli za uchaguzi vitakavyorushwa na vituo vya utangazaji.

Utaratibu huu unazingatia Kanuni Za Huduma Za Utangazaji (Maudhui) (Utangazaji Wa Uchaguzi Wa Vyama Vya Siasa), 2015, Kanuni ya 4 (f), (h), (i), 5(b), (d), (e) and (f).

Hatua hii inachukuliwa na Mamlaka ili kuweka utaratibu mzuri wa kufanya kampeni za uchaguzi ziwe za amani na utulivu.

Hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya kituo cha utangazaji kitakacho kwenda kinyume na utaratibu huu..

IMETOLEWA NA:
Mkurugenzi Mkuu
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

No comments: