Sehemu ya Kinu cha Kiwanda Cha Saruji Cha Wazo Hill Jijini Dar es Salaam ambako dawa za kulevya zimeteketezwa jana chini ya uangalizi mkali . Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzichoma moto katika kinu hicho Jaji wa Mahakama Kuu Edison Mkasimongwa alizitaja aina ya dawa hizo kuwa ni Heroine mifuko 179 na Cocaine mifuko 81 zenye thamani ya Shilingi Bilioni tano ambapo zilikuwa na Gram 175,000 ambazo zilikamatwa miaka kadhaa Mbezi Jogoo jijini Dar.
Jaji wa Mahakama Kuu Edison Mkasimongwa(kulia) akihakiki sehemu ya kinu cha kuchomea madawa hayo ya kulevya uku akisindikizwa na Mkurugenzi wa Mashtaka Biswalo Mganga(kushoto) katika Kiwanda Cha Saruji Cha Wazo Hill Jijini Dar es Salaam
Hii ndio sehemu ya mfuniko wa kinu kilichotumika kuchomea dawa za kulevya
Majaji kutoka mahakama kuu pamoja na polisi wakifuatilia kwa umakini uteketezaji wa dawa za kulevya
No comments:
Post a Comment