.

.
TZ WAKA BLOG TUNAKUTAKIA HERI YA MWAKA MPYA 2016, MWAKA HUU UWE WA BARAKA NA MAFANIKIO KWAKO | KUTANGAZA NA BLOG HII WASILIANA NASI KUPITIA 0716 979 939 AU BARUA PEPE tzwakablog@gmail.com

15 December, 2015

MASHABIKI NA SIFA KEDEKEDE KWA MWANAMUZIKI AY JUU YA HILI

12331683_1007956949264144_2112653779_nKwa AY ni tofauti, na ndio maana bado ameendelea kuwa msanii anayeheshimiwa zaidi si tu na mashabiki, bali wasanii wenzake pia.
Rapper huyo ambaye yupo nchini Afrika Kusini, alipost picha kwenye Instagram na Facebook akiwa amezishika tuzo za MTV alizoshinda Diamond hivi karibuni na kuandika:
Nilichokuwa nakipigania tangu mwanzo nazidi kuona matunda yake na najisikia faraja sana. Sasa kabla hazijatua Tanzania lazima tuzibariki kwanza,Congrats once again Diamond Platnumz kwa awards hizi kubwa za ‪#‎MTVEMA2015‬. Mambo makubwa ya kushtukiza yatakujia soon
 Tazama baadhi ya comments za mashabiki wakimsifu AY kwa moyo wake huo.

Richard Claud
"Napenda sana ulivyo na roho isiyokuwa na wivu hata kidogo ndo maana unafanikiwa kila siku siyo tu kimziki hata kibiashara na hustle zote unazozifanya. Ulikuwa wa kwanza kushoot international video tukashangaa sana lakini kumbe ndo ulikuwa unawaonyesha wasanii wenzako njia na nia ya kuthubutu. Love u more our star..... #HolidaySeason hatari sana"

Yussouf J. Magige
"Wewe ndo umeanzisha safari hii kubwa ya kujaribu kuutoa music wetu nje ya nchi na kupitia wewe tumempata mwingine ambae ni diamond. Nawatakia kila la heri wewe na wadogo zako ambao wana hamu ya mafanikio kama wewe. Nawaombea sana"

Juma Mkelemi Wasasa
"A.Y! A.Y! A.Y! A.Y! unique artist mwenye moyo wa upendo na ndomana pia kazi zako 2nazipenda hasa mm hapa nashangaa sana wasanii wengine kukicha wao ni madongo2 kwa #Diamond why? kwan hzo 2zo amejipa? jaman fanz mm nampenda xna A.Y namfatilia toka miaka ile ya #East_Coast nakumbuka 2005 nlipelekwa kwa mwenyekiti wa mtaa baada ya kumponda kipondo dogo mwenzangu kwa kuiponda nyimbo ya #yule_by_A.Y mama alinilipia faini ya Tsh.5000"

No comments: