Ndugu zangu,
Watanzania huwa hawapendi kuambiwa kwa maneno makali hata kama wanachoambiwa ni ukweli. Tofauti ya aliyemtangulia, Mzee Mwinyi, Mkapa huwa hawezi kurembaremba maneno. Ben ni mwanadiplomasia, lakini, wakati mwingine diplomasia yake ni ya Ki-gunboat fulani, ya kutanguliza makombora kumtisha aliye mbele yake...na akibanwa anaweza kuwa kama mbogo.
Akihojiwa na Tim Sebastian kwenye ' Hard Talk' 2001 kuhusiana na machafuko ya Zanzibar, Mkapa hakupenda maswali ya Tim ( Huenda aliona ni ya kipumbavu!). Mkapa Alionyesha hasira, na Tim Sebastian akamuuliza; " Mr President, are you angry?" Ben Mkapa akajibu; " Yes, I am" huku akionyesha hasira...
Mjadala uendelee..
Kumbukumbu ya Nukuu KHY:
(Maggid, Mwenyekiti.(P.T)
No comments:
Post a Comment