Rais wa Sudan Omar Al Bashir
Kikosi kimoja maalum cha serikali nchini Sudan kimeshutumiwa kwa kutekeleza maujai ya halaiki na ubakaji wa raia katika eneo la Darfur Magharibi tangu mwezi Februari mwaka uliopita.
Ripoti mpya ya Shirika la kutetea haki za Kibinadamu Human Rights Watch inasema kikosi hicho kijulikanacho kama Rapid Support Forces kilitekeleza kile inachosema ni unyama na ukatili katika vijiji tofauti kwenye eneo hilo.
Walioshuhudia mashambulio hayo wameelezea jinsi vikosi hivyo maalum vya serikali viliwakusanya raia katika vijiji, vikaanza kuwapiga na kuwabaka wanawake wengi. Mmoja wa waathiriwa alisema alishuhudia wanawake kumi na saba wakibakwa katika hospitali moja.
Mwingine alisema aliwaona wanawake na wasichana wakibakwa na kasha kuingiza katika nyumba moja iliyochomwa bado wakiwa ndani
No comments:
Post a Comment