Mapenzi ya mwimbaji wa R&B Juma Jux na Vanessa Mdee a.k.a Vee Money sasa yamefikia kwenye ‘climax’. Licha ya kukiri hadharani kuhusu uhusiano wao lakini sasa kila mmoja wao amekuwa tayari kuelezea jinsi anavyompenda mwenzie hadharani ikiwa ni ishara ya kuwa mahaba yako kileleni.
Jux katika kusheherekea siku yake ya kuzaliwa ambayo ilikuwa ni Sept 1, aliamua kuifanya kuwa siku maalum kumuandikia barua ya mapenzi Vanessa, lakini haikuwa barua ya kawaida kama tulivyozoea bali ni barua ya moyo wake kumzungumzia jinsi alivyobadili maisha yake toka wamekuwa wapenzi.
“Tomorrow is my birthday nitaifanya maalum kwa msichana aliye badilisha maisha yangu. Nitaiweka wazi barua ya moyo wangu ambayo huwa naisoma kila siku kwenye nafsi yangu.” Aliandika Jux Instagram siku moja kabla ya birthday yake.
No comments:
Post a Comment