.

.
TZ WAKA BLOG TUNAKUTAKIA HERI YA MWAKA MPYA 2016, MWAKA HUU UWE WA BARAKA NA MAFANIKIO KWAKO | KUTANGAZA NA BLOG HII WASILIANA NASI KUPITIA 0716 979 939 AU BARUA PEPE tzwakablog@gmail.com

01 September, 2015

Neno Kwa Neno Katika yale aliyozunguza Dr.Slaa kwenye Mkutano na waandishi wa Habari Leo.

...Slaa akizungumza jambo mbele ya wanahabari juu ya hatma yake ya kuachana na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo....
-Asema lazima ajitokeze kusema na kuweka ukweli hadharani
-Asema sina tabia ya kuchengachenga nasimamia ninachokiamini
-Mengi yamesemwa na kuandikwa magazetini
-Sina ugomvi na kiongozi yoyote, maana siasa si ugomvi, sina chuki, sina hasira na mtu yeyote
-Siasa inayoongozwa na propaganda, ulaghai ni kuleta vurugu katika taifa na nimekataa hayo
yote.
-Ni kweli nilishiriki katika majadiliano tangu mwanzo
-Misingi niliyoweka ni kwamba Lowassa atangaze kuwa ameachana na chama chake na aeleze anakwenda chama gani kwanza na ajisafishe na tuhuma zake
-Asema hawezi kumsafisha mtu bila yeye kufanya hivyo
-Asema alihoji kama Lowassa anakuja Chadema kama faida au mzigo (assets au liability)
-Asema anataka mgombea mwenye uwezo, sifa na kuiongoza Chadema kuiondoa CCM.
-Kama ni assets anakuja na akina nani? vijana wa mitaani, bodaboda au watu wa aina gani? ni viongozi makini?
-Asema aliambiwa kuwa anahama na wabunge 50, wenyeviti wa mikoa 22, wenyeviti wa CCM wilaya 82.
-Sikupewa majina ya wabunge wala wenyeviti.
-Nikatakiwa kuitisha kikao nikaitisha lakini sikuwa na majibu kama Lowassa ni
Assets au Liability.
-Tangu 2004 sikuwahi kutofautina na mwenyekiti wangu bali tulitofautia kwa hilo.
- Asema aliandika barua ya kujiuzulu kwa M/kiti Prof. Safari barua ikachanwa.
-Siasa ni sayansi haitaki uongo wala ulaghai au propaganda
-Asema mke wake halipwi chochote kutoka Chadema na amekuwa akizunguka nchini kwa mshahara wa Dk. Slaa.

No comments: