.

.
TZ WAKA BLOG TUNAKUTAKIA HERI YA MWAKA MPYA 2016, MWAKA HUU UWE WA BARAKA NA MAFANIKIO KWAKO | KUTANGAZA NA BLOG HII WASILIANA NASI KUPITIA 0716 979 939 AU BARUA PEPE tzwakablog@gmail.com

08 September, 2015

NUHU MZIWANDA: "SIONI TATIZO LA MSANII KUONYESHA MAHABA KWA CHAMA ANACHOKIPENDA."

Msanii wa Bongo Fleva Nuhu Mziwanda amewataka wasanii kuwa wazalendo kwa kuonyesha hisia zao za vyama vya siasa na kuonyesha ushirikiano katika kuhamasisha.


Akizungumza na Planet Bongo ya East Africa Radio leo, Nuh alisema maendeleo yatakayopatikana ni manufaa kwa watanzania wote kwa ujumla. 

“Wewe ukiwa msanii sio kwamba sio mwananchi wa kawaida,” alisema. 

“Wewe pia unahitaji kutawaliwa vizuri. Unahitaji utawala mzuri ambao utaongoza hata kazi zako ziende vizuri.
 Kwahiyo ni vyema mtu ukajua upo upande gani, huo ni upendo wa nchi yako na ni mzalendo. Kila binadamu anapenda uongozi mzuri ndio maana kila mtu akiwa na akili timamu ana haki ya kuchagua chama anachokitaka,” aliongeza. 


“Lakini sisi wasanii tusijisahau tukawa tunashindwa kuweka hisia zetu kwaajili ya maslaHi ya nchi yetu. Unaogopa kuweka wazi wewe ni chama gani, unampenda mwanasiasa gani! Sisi ni vioo vya jamii tunaangaliwa pia na watu na kuna watu wahitaji ushauri au ufafanuzi juu ya viongozi waliotangaza nia. Kwa sisi inatubidi tuwe mfano kwanza kabla ya wananchi.”

No comments: