.

.
TZ WAKA BLOG TUNAKUTAKIA HERI YA MWAKA MPYA 2016, MWAKA HUU UWE WA BARAKA NA MAFANIKIO KWAKO | KUTANGAZA NA BLOG HII WASILIANA NASI KUPITIA 0716 979 939 AU BARUA PEPE tzwakablog@gmail.com

04 September, 2015

SABABU YA LEMA KUSWEKWA RUMANDE JANA

Mgombea ubunge jimbo la Arusha Mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na UKAWA, Godbless Lema na wenzake wanne wameachiliwa kwa dhamana leo baada ya kushikiliwa na polisi tangu jana.
Polisi mkoani Arusha waliwakamata watuhumiwa hao jana jioni mara baada ya kuzindua kampeni ya kuwania ubunge katika jimbo hilo katika Shule ya Msingi Ngarenaro.
Wakisomewa mashtaka katika mahakama ya Arusha, Lema amedaiwa kulizima gari lake wakati wakitokea kwenye mkutano wa kampeni, hali iliyowafanya wafuasi wake kuanza kulisukuma hivyo kusababisha maandamano pasipo kuwa na kibali cha polisi. Lema na wenzake wameyakana mashtaka dhidi yao.

No comments: