THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telegrams : "CABINET"
DAR ES SALAAM
Telephone : 2116898, 2116900/6
E-mail : chief@ikulu.go.tz
E-mail : ikulu@ikulu.go.tz
Fax : 2113425/2116914/2117272
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD
11400 DAR ES SALAAM.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo asubuhi katika Ikulu ya Dar esSalaam amefanya kikao na Makatibu wakuu, Manaibu Makatibu wakuu, Gavana wa Benki Kuu Prof.Benno Ndulu na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilikutoa uelekeo wa Serikali anayoita kamara baada ya kuapishwa.
“Nataka Serikalii endelee kwanguvu zote na katika kutekeleza dhana ya‘HAPA KAZI TU’naviongozi kuzingatia na kukumbuka ahadi nilizotoa ili zianze kuonekana na kufanyiwa kazi mara moja” Rais Magufuli amesema.
Katika Kikao chake, Rais ametoa mwongozo na kusisitizia kuwa nilazima kilamtendaji Serikalini kuuzingatia, kufuata sheria na taratibu ili taifa lisonge mbele kwa ufanisi zaidi.
Katika kikao hicho Rais ameelekeza mambo kadhaa ambayo watendaji hao wanapaswa kuyasimamia, kuyawekea mikakati na kuyapanga vizuri ili atakapoteua Baraza lake la Mawaziri mambo hayo yawe tayari ili Mawaziri watakao teuliwa waweze kuyasimamia bila kukosa.
Mambo hayo muhimu ni kamaifuatavyo:
Kuanzia mwezi Januari mwaka 2016, wanafunzi wote wanaoanza shule watasoma bure bila kulipa ada, Katika jambo hili, Rais amewataka watendaji kuanza kuliwekea mikakati tayari kwautekelezaji
Suala la mikopo yawanafunzi nalo lifanyiwe kazi na mipango yake ikamilike kwa ajili ya utekelezaji mzuri zaidi
Amefuta safari zote za nje ya nchi kuanzia leo hadi hapo atakapo litole asuala hilo maamuzi mengine na kueleza kuwa shughuli zote zinazotakiwa kufanywa nje ya nchizifanywe na kusimamiwa na mabalozi wa Tanzania wanao wakilisha nchi huko nje.
Pengine patokee jambo la dharura sana na hata hilo lazima kibali kitolewe na Rais au Katibu Mkuu Kiongozi. Badala yake Rais amewataka watendaji hao kufanya zaidi ziara za kwenda vijijini ili kuzijua na kutatua kero za wananchi wa Tanzania.
Katika Kikao hicho, Rais amemtaka Kamishna wa TRA, Ndugu Rished Bade kusimamia kwa makini zoezi la ukusanyaji wa mapato nchini na kuhakikisha kero ndogo ndogo kwa wananchi lianzekutekelezwa kama alivyo ahidi kwa kufanyiwa kazi mapema zaidi.
Rais ameitaka TRA kukusanya mapato hayo kutoka kwa wafanyabiashara wakubwa zaidi na wale wanaokwepa kodi bila kuogopa mtu wala taasisi yoyote hapa Tanzania na kusisitiza kuwa katika Serikali hii wakuto amaamuz ivinginevyo zaidi ya haya ni yeye Rais ama Makamu wake.
Rais Magufuli pia ameagiza usimamizi katika suala la manunuzi ambalo limekuwa likitumika vibaya na kuwa mwanya wa kuibia Serikali kwa watu kuongeza bei ya vitu hata kama ni vya bei ndogo kabisa katika jamii.
“Ikitokea suala hilo likagundulika kwa watu kuongeza bei ya vitu, watendaji watawajibishwa mara moja”. Rais amesema, nakuwataka watendaji hao kufanya kazi zao kwa kuzingatia Sheria na taratibu zilizopo na kuzingatia maadili mema yakazi.
………………………MWISHO……………………
Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
7 Novemba, 2015 .
No comments:
Post a Comment