Wasanii Q Chief na MB Dog,wanaosimamiwa na meneja mwezeshaji QS J Mhonda anatarajia kuwarudisha shule wanamuziki hao.
Akiongea na Planet Bongo ya East Africa Television, Mhonda alisema hatua hiyo itawasaidia wasanii hao kuweza kujitegemea nje ya muziki.
“Nataka kuwapeleka katika fani mbalimbali kama ujenzi, uchoraji na fani nyingine. Q Chief na MB Dog nao wataenda kujifunza ili waweze kufanya ishu nyingine nje ya muziki”, alisema Mhonda.
QS J Mhonda ni moja ya kampuni kubwa za muziki nchini zinazotumia gharama kubwa katika kusimamia wasanii wake pamoja na kuwagharamikia kwa vitu mbalimbali.
No comments:
Post a Comment